Kiungo mshambuliaji mahiri, Stephane Aziz Ki, sasa ni mchezaji halali wa klabu ya Wydad Athletic ya Morocco baada ya kutambulishwa rasmi na vigogo hao wa Afrika Kaskazini. Ki amejiunga na Wydad akitokea klabu ya Yanga ya Tanzania, ambako aliwika kwa kiwango bora na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Wanajangwani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Wydad, Aziz Ki amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo inajiandaa kwa nguvu kuelekea michuano ya Kombe la Dunia la Klabu. Usajili huu ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha kikosi cha Wydad kuelekea mashindano hayo ya kimataifa.
Mbali na Aziz Ki, Wydad pia imetambulisha nyota wengine wawili wapya: mshambuliaji mwenye uzoefu mkubwa, Nordin Amrabat, aliyewahi kung’ara katika Ligi Kuu ya Hispania na timu ya taifa ya Morocco, ambaye amejiunga na Wydad akitokea AEK Athens ya Ugiriki, pamoja na Hamza Hanouri kutoka klabu ya FUS Rabat ya Morocco.
Kwa upande wake, klabu ya Yanga imetoa salamu za heri kwa Aziz Ki, ikimtakia mafanikio mema katika changamoto yake mpya. Kupitia mitandao ya kijamii, Yanga imempongeza Ki kwa huduma aliyotoa akiwa na timu hiyo, huku mchezaji huyo naye akiishukuru klabu, wachezaji wenzake na mashabiki kwa kipindi kizuri alichokipitia akiwa Jangwani.
Aziz Ki anasalia kuwa mmoja wa wachezaji wa kigeni waliovutia sana katika Ligi Kuu ya Tanzania, na sasa macho yote yataelekezwa kwake kuona atakavyoweza kuonesha uwezo wake katika jukwaa la kimataifa akiwa na Wydad.
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment