Wakati zikisalia wiki chache kabla ya msimu kumalizika na dirisha la usajili kufunguliwa, Yanga tayari inahusishwa na nyota kadhaa
Katika maeneo ambayo yanatarajiwa kuboreshwa ni pamoja na safu ya ulinzi ambapo Yanga inatarajiwa kuongeza beki mwingine wa kati ambaye atashirikiana na mabeki waliopo Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto
Jina la beki wa Kimataifa wa DR Congo Hennock Inonga Baka ni miongoni mwa majina ya wachezaji wanaotajwa kufuatiliwa ili kusajili
Inonga aliitumikia Simba kwa misimu mitatu kabla ya kutimkia klabu ya FAR Rabat ya Morocco anayoitumikia sasa
Hata hivyo tetesi za Yanga kutanga kumsajili beki huyo zimeibua mjadala mzito wengi wakihofia mwendelezo wa wachezaji waliosajiliwa na Yanga kutoka Simba kutofikia matarajio ya mashabiki
Katika misimu ya karibuni Yanga iliwasajili wachezaji kama Jonas Mkude, Jean Baleke, Augustine Okrah, Clatous Chama na Israel Mwenda
Mkude, Chama na Mwenda bado wapo huku Baleke na Okrah wakiitumikia Yanga kwa miezi 6 tu kabla ya mikataba yao kuvunjwa
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa gazeti la Mwanaspoti, baadhi ya viongozi wa Yanga hawataki kabisa kusikia suala la kumsajili mchezaji yeyote aliyewahi kuichezea Simba
Wanahoji kwamba mara nyingi mastaa wanaotoka kwa wapinzani wao hao hawajathibitisha ubora wao walipotua Jangwani
Mtoa taarifa kutoka ndani ya Yanga alinukuliwa akisema:
"Baadhi ya mabosi wamechoka mazoea ya kuchukua wachezaji kutoka kwa wapinzani wetu wakubwa wakati mastaa wapo wengi tu... wengine wanahisi Inonga anaweza kufanya makosa na ikatafsiriwa kama hujuma kwa sababu ya historia yake na Simba"
Ukitoa hofu hiyo, Inonga amedhihisha ubora wake akiwa beki tegemeo katika timu ya Taifa ya DR Congo na ameendelea kuaminiwa katika kikosi cha FAR Rabat licha ya kukabiliwa na ushindani katika kikosi cha kwanza
Usikose kuzitazama mechi ya YANGA vs NAMUNGO LIVE bure kupitia simu yako download App yetu muda huu inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment