Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga kesho Jumatatu Februari 17 watakuwa na nafasi ya kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi pale watakapoikabili Singida Black Stars katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex
Katika msimu ambao Yanga imepania kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo, ushindi dhidi ya Singida BS ni matokeo muhimu hapo kesho
Singida BS ni timu isiyotabirika, waliipa Yanga upinzani mkali katika mechi ya duru ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar licha ya Yanga kushinda mchezo huo kwa bao 1-0
Ni kweli Yanga na Singida BS zina mahusiano mazuri ya kiungozi nje ya uwanja lakini timu hizo zinapokutana uwanjani nyasi huwaka moto
Singida BS ina wachezaji wengi wa Kimataifa kama ilivyo Yanga, mechi za aina hii wanazipenda kwa sababu huwatangaza zaidi na pengine zinaweza kuwapa nafasi ya kuhama kutoka Singida kuja mjini!
Ili kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa, kuna mechi tatu muhimu ambazo lazima Yanga ishinde
Mchezo wa kwanza ni dhidi ya Singida BS, mchezo mwingin ni dhidi ya Azam Fc na mchezo dhidi ya Simba
Hizi ni alama 9 ambazo zinaweza kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
Au hapa chini
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment