TETESI za Usajili Simba SC dirisha dogo la Usajili 2024/2025
![Feisal Salum Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/12/GUuJO8zWcAE52Mz-1024x851-1.jpg)
Feisal Salum Simba SC
Rais wa heshima na Mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ amewasilisha ofa ya dola 300,000 (Zaidi ya milioni 730 pamoja na golikipa Aishi Manula kwa maboss wa Azam FC, ili kumpata kiungo mshambuliaji, Feisal Salum Abdallah.
![Imourane Hassane Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/12/20241231_094040.jpg.webp)
Imourane Hassane Simba SC
Klabu ya Simba SC unaangalia uwezekano wa kumpata Kiungo, Imourane Hassane mwenye umri wa miaka 21 Kutoka Loto-Popo FC ya nchini kwao Benin katika dirisha hili dogo la usajili.
Kiungo huyo pia ananyatiwa na Kaizer Chiefs pamoja na Zamalek,
![Karim Kimvuidi Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/11/karim-kimvuidi-midfielder-home-headshot-2024-25-kit-brandon-barnard-photography-L1040653-op-1-1.webp)
Karim Kimvuidi Simba SC
Klabu ya Simba SC imetajwa kutuma ofa kwenda Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwaajili kumpata Kiungo, Karim Kimvuidi raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 22 katika dirisha hili dogo la usajili.
Usikose kuitazama mechi ya AL HILAL 🆚 YANGA na BRAVO 🆚 SIMBA LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee
![Fabrice Ngoma Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/12/20241115_082040-1024x1024-1.jpg.webp)
Fabrice Ngoma Simba SC
Uongozi wa klabu ya Simba SC umefanya mawasiliano na wakala wa kiungo Fabrice Ngoma (Fausty Mkandila) na kufikia Makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia Simba SC.
![Abdelhay Forsy Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/11/771677579.jpg)
Abdelhay Forsy Simba SC
Simba SC inamfuatilia kwa ukaribu kiungo mshambuliaji, Abdelhay Forsy mwenye umri wa miaka 26 na huenda akatua klabuni hapo katika dirisha hili dogo.
Forsy ambaye yupo RCA Zemmra Kwa Mkopo akitokea Raja Athletic ya Morocco ni moja ya majina matatu ya viungo washambuliaji ambao Fadlu Davids anaohitaji kujiunga na Simba.
![Ayoub Lakred Simba SC](https://www.nijuzehabari1.com/wp-content/uploads/2024/11/04895b77-9fac-4482-859b-1a0972dc6548-1024x732-1.jpg)
Ayoub Lakred Simba SC
Uongozi wa klabu ya Simba SC, umesema kuwa upo tayari kumwachia golikipa Ayoub Lakred kwenye dirisha hili dogo la usajili.
Ayoub ambaye alikuwa majeruhi tangu msimu huu uanze anatakiwa na vilabu vya JS Kabylie ya Algeria na Raja Casablanca ya Morocco.
Post a Comment