Simba kurejea Dar Jumatano
Usikose kuitazama mechi ya SIMBA vs AL AHLI TRIPOLI Live bure kwenye simu yako download app yetu itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii bure kabisa pia ukiwa na app yetu utweza kutazama chanel za AZAM TV na DSTV bure kabisa pia na mechi zote za Nbc premier league na mechi zote za Ulaya kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) dhidi ya Al Ahli Tripoli, kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini siku ya Jumatano
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema leo timu itaendelea na maandalizi yake hapo Tripoli kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania
"Baada ya mchezo wetu dhidi ya Al Ahli Tripoli, timu bado iko hapa Libya na tutarejea Tanzania siku ya Jumatano. Wachezaji wameendelea na program maalum za mazoezi ambapo jana timu ilifanya mazoezi maalum ya recovery"
"Leo timu itafanya mazoezi asubuhi na mchana kuanza safari kurudi nyumbani ambapo tutapitia Uturuki kuunganisha ndege ya moja kwa moja Tanzania," alisema Ahmed
Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Jumapili, Septemba 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni
Simba itahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kufuzu hatua ya makundi
No comments:
Post a Comment