Klabu ya Simba imeachana na mpango wa usajili wa beki Lameck Lawi kutoka klabu ya Coastal Union, imefahamika
Lawi amerejea nchini hivi karibuni baada ya mpango ya kujiunga na KAA Genk ya Ubelgiji kukwama
Mchezaji huyo aliingia kwenye mgogoro baada ya kusaini klabu ya Simba wakati huohuo klabu yake ya Coastal Union ikigoma kumuachia kwa madai Simba haikukamilisha mchakato wa usajili wake kwa wakati
Simba ilipeleka malalamiko yake Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji lakini taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba imethibitisha kuwa Wekundu hao wa Msimbazi wamefuta shauri hilo
Simba imechukua uamuzi huo kwa kile kilichoelezwa kuzingatia maslahi ya mchezaji ili kumruhusu aendeleze kukuza kipaji chake
Lawi (18) alipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nchini Ubelgiji hata hivyo hakufanikiwa
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment