Itakuwa kama vita pale uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili, Septemba 22 katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Majira ya saa 10 jioni Simba itakuwa mbele ya mashabiki wake kusaka ushindi utakaowapeleka hatua ya makundi Wekundu hao wa Msimbazi
Ni Jumapili ya kuwakaanga! Kila Mwanasimba anapaswa kufahamu hivyo kwani yanahitajika matokeo ya aina moja tu, USHINDI
Kila Mwanasimba kindakindaki ambaye yuko jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani anapaswa kuwa dimba la Mkapa, kuwaongezea hamasa wachezaji
Lengo ni kuhakikisha mashabiki 60,000 wanaingia uwanjani kuwashushia pumzi ya moto 'wamanga' hao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametangaza, Jumapili makutano ya Wanasimba ni dimba la Mkapa
Mwamba kabisa, kiungo fundi Yusuph Kagoma amepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo...!
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment