Winga wa zamani wa AS Vita Club Elie Mpanzu yuko nchini kukamilisha taratibu za usajili wake na Simba, imefahamika
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amethibitisha kuwa Mpanzu yuko nchini ambapo amebainisha iwapo Simba itakamilisha usajili wake basi watakuwa wameongeza ubora kwa washambuliaji wanaotokea pembeni
"Mpanzu ni mchezaji hatari na mimi nimesikia tayari yuko jijini Dar es salaam. tunao wachezaji wazuri wa pembeni kina Edwin Mbalua, Kibu Denis, Ladack Chasambi na Joshua Mutale"
"Siku hizi pembeni kuna mchango mkubwa wa mafanikio ya kupata magoli kwa hiyo niseme wazi wachezaji wanayo nafasi ya kuboresha kiwango chao ili mwalimu awe na Imani kubwa nao"
"Kama ikitokea Tumemsajili Mpanzu basi litakuwa jambo zuri kwasababu hao vijana wote niliyokutajia bado kwa namna yake wanahitaji uzoefu kwa wakongwe kama Mpanzu," alisema Ahmed
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba imebainisha kuwa Rais wa heshima Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndye aliyefanikisha ujio wa Mpanzu ambapo atakamilisha usajili wake kisha ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Simba akisubiri dirisha dogo la usajili kufunguliwa ili asajiliwe rasmi katika mfumo
No comments:
Post a Comment