Jeuri ya Yanga kwa Mzize iko hapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mshambuliaji Clement Mzize amechagua kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa nchi kutokana na mipango mizuri waliyonayo
Hivi karibuni Yanga ilipokea ofa kutoka kwa klabu za Wydad Athletic, Kaizer Chiefs na nyingine kutoka barani Ulaya kwa ajili ya mshambuliaji huyo kinda
Hata hivyo Yanga iliweka msimamo na kukataa ofa zote wakisisitiza kuwa mchezaji huyo anahitajika katika kufanikisha 'project' ya Yanga
"Kumbakisha Mzize ni moja kati ya mipango tuliyokuwa nayo katika klabu yetu ya Yanga. Mzize ni mchezaji mzuri sana ambaye tunaamini anaweza kuisaidia Yanga ikafikia malengo yake ambayo ni kutwaa ubingwa wa Afrika"
"Ikitokea hii leo Mzize au mfano hata Aziz Ki amesajiliwa na Al Ahly na timu hiyo ikabeba ubingwa wa Afrika, wao binafsi hawawezi kusema kawapa kombe na haitokuwa ajabu sana kwa sababu wameshatwaa kombe hilo mara 11. Lakini mshawahi kujiuliza kama Mzize anabeba kombe la Afrika na Yanga kwa mara ya kwanza katika historia ni kitu ambacho kitampa heshima kubwa kama mchezaji"
"Lakini pia sisi tunasema hatumuuzi Mzize kwa sababu tunaweza kumtimizia mahitaji yake. Hatuwezi kuwa na jeuri hiyo kama tusingekuwa na fedha," alitamba Kamwe
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment