Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza jambo muhimu kwa kikosi chake ni alama tatu kwani sio kila mechi watafunga idadi kubwa ya mabao
Yanga iliichapa KMC bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopgwa uwanja wa Azam Complex, ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo Yanga ikifunga bao bao moja
Akizungumza baada ya mchezo huo Gamondi aliwapongeza wachezaji wake kwa ari kubwa walioingia nayo katika mchezo huo lakini pia hakusita kuwapongeza wapinzani wake KMC kwani walikuwa madhubuti katika kujilinda
"Mimi nimefurahi kwa sababu tumeshinda, muhimu ilikuwa alama tatu. Wachezaji walicheza vizuri tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wetu"
"Nawapongeza KMC pia, walikuwa na nidhamu kubwa katika kujilinda, kipa wao amefanya kazi nzuri"
"Alama tatu ndio jambo muhimu kwetu, tungeweza kufunga mabao mawili au hata matatu lakini nafikiri kipa wa KMC alikuwa na siku nzuri sana leo (jana)"
"Kwangu mimi sio tatizo kushinda bao moja, inanishangaza Yanga inaposhinda bao moja mnasema lakini timu nyingine zikishinda moja mbona hamzungumzi?. Ni timu ngapi zimeshinda bao moja kwenye ligi msimu huu?", alihoji Gamondi
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Pamba Jiji na utapigwa Alhamisi, Oktoba 03 katika uwanja wa Azam Complex
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment