CBE wameandaliwa dozi New Amaan Complex
Jumamosi Septemba 21 Yanga inakwenda kukamilisha mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA
Kikosi cha kocha Miguel Gamondi kitaingia katika mchezo huo kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Kimahesabu Yanga inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga hatua ya makundi
Lakini matarajio ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao inaibuka na ushindi mnono zaidi katika dimba la New Amaan Complex
Yanga ina rekodi nzuri ya kufunga mabao msimu huu ambapo mpaka sasa imepachika mabao 18 katika mechi za mashindano
Washambuliaji Prince Dube na Clement Mzize watakuwa na nafasi ya kuendeleza kasi yao ya kufunga kila mmoja akiwa amepachika mabao manne
MVP wa ligi kuu msimu uliopita Stephane Aziz Ki mpaka sasa amefunga mabao matatu huku Clatous Chama na Maxi Nzengeli kila mmoja akifunga mabao 2
Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya nao ni miongoni mwa wachezaji waliopachika mabao ambapo kila mmoja amefunga bao 1
CBE SA walinusurika na kipigo kizito katika uwanja wao wa nyumbani kwani licha ya kufungwa bao 1 tu, Yanga ilipoteza takribani nafasi saba
Pengine Jumamosi wanaweza kukumbana na kile kilichowakuta Vital'o kama hawatakuwa makini
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment