Wafahamu CBE, wapinzani wa Yanga kwenye CAFCL
Usikose kuitazama mechi ya KAGERA SUGAR vs YANGA live bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuitazama mechi hii live bure pia ndani ya app yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na DSTV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Commercial Bank of Ethiopia Sports Association (CBE SA) ni Klabu ambayo ilianzishwa mwaka 1982 nchini Ethiopia ikiitwa Banks SC.
Mwaka 2010 ilibadilishwa jina na kuitwa Commercial Bank of Ethiopia Sports Association (CBE SA) ndilo wanalotumia mpaka sasa. Pia wana jina lao la utani wanaitwa Ethiopia Nigb Back.
Klabu hii inashiriki Ligi Kuu ya nchini Ethiopia na ndio mabingwa wa ligi hiyo kwa msimu uliopita 2023/24.
Inapatikana kwenye jiji la Addis Ababa, Ethiopia. Inatumia uwanja wa Addis Ababa Stadium kwenye michezo yao ya nyumbani.
Kwenye michuano ya ndani mafanikio yao makubwa ni ubingwa wa ligi hiyo walioupata msimu uliopita,pia mwaka 2014 walishinda ubingwa wa Addis Ababa City Cup.
USHIRIKI WAO KIMATAIFA ...Hawajawahi kushiriki michuano ya klabu bingwa katika historia yao, msimu huu ni wa kwanza kwao.
Kombe la shirikisho barani Afrika Wameshiriki mara 2 hajawahi kufika hatua ya makundi. 2005-Raundi ya kwanza 2010- Raundi ya kwanza.
Yanga wataanza ugenini na kumalizia nyumbani, wautatumia uwanja wa New Amaan Zanzibar.
Michezo ya hatua hii ya pili klabu bingwa Afrika, kwa mzunguko wa kwanza itachezwa kati ya tarehe 13-15 mwezi wa 9 na marudiano ni kati ya tarehe 20-22 mwezi wa 9.
Wapinzani wa Yanga kutoka Ethiopia Klabu ya CBE (Commercial Bank of Ethiopia) msimu huu ndio wanashiriki kwa mara ya kwanza ligi ya Mabingwa Afrika.
Hii ikiwa baada ya kubeba pia ubingwa wao wa kwanza wa ligi kuu ya Ethiopia katika msimu wa mwaka 2023/24. Klabu hiyo imeanzishwa mwaka 1982 inapatikana katika mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa.
Katika kombe la Shirikisho Afrika imeshiriki mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote imetolewa katika hatua ya awali.
Msimu huu ukiwa wa kwanza kushiriki ligi ya Mabingwa Afrika wanafanikiwa kusonga mbeke kwa kumtoa SC Villa ya Uganda kwa uwiano wa mabao ndio mafanikio makubwa kwao kimataifa Wanaenda kukutana na Yanga mechi ijayo.
Yanga Africa haijawahi kushinda nchi ni Ethiopia kwenye michuano ya vilabu Afrika wanapokutana na timu za nchi hiyo nchini kwao na msimu huu hatua inahofuata huenda wakaminyana na CBE ambao walishinda 2-1 dhidi ya SC Villa Ya Uganda
CAF Champions League 1969 ST George 0-0 Yanga 1998 Coffee 2-2 Yanga
CAF CC 2011 Dedebit 2-0 Yanga 2018 Walauta Dicha 1 - 0 Yanga.
licha ya kuwa Kwenye Matokeo ya Jumla Yanga wamekuwa wababe kwani katika mara nne walizominyana na miamba ya Ethiopia mara tatu Yanga ilisonga mbele kutokana na matokeo mazuri wanayoyapata Nyumbani huku mara moja wakitupwa mashindanoni.
No comments:
Post a Comment