Kibu arejea, kupelekwa Kamati ya nidhamu
Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis amerejea nchini akitokea Norway ambako alikwenda kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa
Kibu aliondoka nchini pasipo ruhusa ya uongozi, amerejea na moja kwa moja kujiunga na wenzake kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea Simba Day sku ya Jumamosi
Hata hivyo Kibu atalazimika kujitetea katika Kamati ya Nidhamu kutokana na sintofahamu aliyosababisha
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amethibitisha ni kweli Kibu amerejea na hatma yake iko mikononi mwa uongozi
"Kibu Denis ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu hali ya juu. Pamoja na haya yaliyotokea, sisi tunatambua Kibu ni kijana wetu mtiifu"
"Iko nafasi kwa sisi kuzungumza na kijana wetu, tukaweka sawa na mchezaji wetu akaendelea kuitumikia Simba," alisema
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment