Hasheem Ibwe: Azam tumelitia aibu Taifa
Usikose kuitazama mechi ya KAGERA SUGAR vs YANGA live bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuitazama mechi hii live bure pia ndani ya app yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na DSTV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA
Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amekiri timu hiyo kulitia aibu Taifa, kwani ilikuwa ikitarajiwa kuibuka na ushindi mnono.
Ameyasema hayo baada ya matajiri hao wa Jiji kutolewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika hatua ya mtoano kwa kufungwa mabao 3-1 kwa matokeo ya jumla na APR ya Rwanda.
"Tumewaangusha mashabiki wetu, tumewaangusha Watanzania wote tumekuwa aibu kwenye Taifa la watu mbele ya timu ambayo tunaiweza, mbele ya timu ambayo tungeweza kupata ushindi nyumbani na ugenini.
"Hatujacheza vizuri hata kidogo mechi zote mbili kuna wakati lazima ukweli mchungu useme tumefedheheka mno. Timu yetu sio mbaya ina ubora wa hali ya juu, lakini tumeondoshwa ugenini.
"Siombi Msamaha leo wala sitetei WE NEED CHANGES ,WE NEED TO CHANGE, Soon Mtafurahi, Azam Itacheza tena ,Azam Itafunga sana Azam Itakuwa Tishio RED BUTTON ON".
Timu hiyo imetolewa kwenye michuano hiyo baada kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini nchini Rwanda na kutoka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani katika mchezo wa awali.
Timu ya Yanga pekee ndio imebakia kuwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada kushinda mabao 10 - 0 dhidi ya Vital’O ya Burundi kwa michezo miwili iliyochezwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi mkoani Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment