Baada ya msimu mmoja wa mafanikio akiwa na Yanga, winga Skudu Makudubela amewaaga rasmi Wananchi baada ya mkataba wake kumalizika
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Skudu ameishukuru familia ya Yanga kwa nyakati mzuri alizopata katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini
"Ninaandika ili kutoa shukrani zangu za dhati kwa Familia nzima ya Yanga kwa upendo mlioonyesha kwangu wakati nikiwa Tanzania"
"Fadhilia na uchangamfu wenu umeacha alama isiyofutika moyoni mwangu. Kwa uongozi wa klabu, hasa Bw. GSM na Rais Bw. Hersi, natanguliza shukrani zangu za dhati kwa imani mliyoonyesha kwangu. Imani yenu imemaanisha ulimwengu kwangu"
"Ni heshima iliyoje kuiwakilisha Taasisi adhimu kama hii. Benchi la ufundi, linaloongozwa na Kocha Miguel Gamondi, imekuwa furaha kabisa kufanya kazi nayo. Ninashukuru kwa nafasi ya kujifunza kutoka kwako na kukua kama mchezaji"
"Kwa wachezaji wenzangu na marafiki, Nyinyi ni askari wa kweli, na nina heshima kuwa nimeshiriki mchezo nanyi. Endelea kuangaza, na Mungu awabariki nyote," aliandika Skudu
Akiwa na Yanga Skudu alifanikiwa kushinda mataji mawili, Ligi Kuu na kombe la FA huku akiwa sehemu ya kikos kilichocheza robo fainali ya ligi ya mabingwa
Kila la kheri Waziri wa raha......!
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment