Siku tatu za bandika bandua utambulisho wa wachezaji Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Siku tatu za bandika bandua utambulisho wa wachezaji Yanga

Siku tatu za bandika bandua utambulisho wa wachezaji Yanga

Usikose kutazama live mechi za EURO 2024 bure kwenye simu yako download app yetu kutazama pia chanel za Azam tv zote bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPAYanga tayari imetangaza kuanzia Jumatatu, wachezaji wataanza kuripoti Avic Town kwa ajili ya taratibu za maandalizi ya msimu mpya wa mashindano, 2024/25

Ndani ya siku tatu Yanga inatarajiwa kuweka hadharani silaha zao zote zinazokwenda kuwapigania Wananchi msimu ujao malengo yakiwa kutetea ubingwa wa ligi kuu na FA kwa msimu wa nne mfululizo, kurejesha Ngao ya Jamii pamoja na kuvuka robo fainali ya ligi ya mabingwa (CAF CL)

Mpaka sasa Yanga imetambulisha mchezaji mmoja tu mpya ambaye ni Clatous Chama na pia ikiendelea kutangaza majina ya nyota ambao wameongeza mikataba

Huenda leo Yanga ikaendelea na zoezi la kutangaza wachezaji walioongeza mikataba na pengine Jumamosi, Jumapili na Jumatatu ikahitimisha kutangaza wachezaji wapya waliosajiliwa

Mpaka sasa wachezaji walioongeza mikataba ni Djigui Diarra, Aboutwali Mshery, Nickson Kibabage, Bakari Nondo Mwamnyeto huku Zawadi Mauya, Metacha Mnata na Augustine Okrah wakipewa mkono wa kwaheri

Wachezaji wengine wanaotajwa kuongeza mikataba ni Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Clement Mzize na Jonas Mkude

Wakati Chadrack Boka, Prince Dube na Jean Baleke wanatajwa miongoni mwa wachezaji wapya wanaosubiri utambulisho

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz