Ni Yanga vs Vital'o Ligi ya Mabingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Ni Yanga vs Vital'o Ligi ya Mabingwa

Ni Yanga vs Vital'o Ligi ya Mabingwa

Usikose kutazama live mechi za EURO 2024 bure kwenye simu yako download app yetu kutazama pia chanel za Azam tv zote bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Droo ya hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika imechezeshwa leo na timu zote zimepangwa.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo, Klabu ya Yanga wamepangwa kucheza na Vital'O ya Burundi ambapo Yanga SC wataanzia ugenini na kumalizia nyumbani.

Yanga akitoboa kwenda hatua ya pili atakutana mshindi kati ya SC Villa ya Uganda vs Commercial Bank ya Ethiopia.

Azam FC wao wamepangwa kucheza na APR FC ya Rwanda ambapo Wauza Ukwaju hao wataanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

Aidha, Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, JKU wao wataanzia nyumbani dhidi ya Pyramids ya Misri anayoichezea Fiston Mayele.

Iwapo Azam atatoboa kwenda hatua ya pili atakutana na mshindi kati ya JKU vs Pyramids.


Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 - 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 - 25, 2024.

Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024.

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz