Baada ya kuachana na kiungo Zawadi Mauya, Yanga inatarajiwa kusajili kiungo mkabaji mwingine ambapo mabingwa hao wa Tanzania Bara wanahusishwa na 'mkata umeme' kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Onoya Sangana Charve (21), anayeichezea Klabu ya AS Maniema
Yanga imedhamiria kufanya vizuri hasa katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao hivyo inaimarisha kila idara ili kuwa na kikosi kipana mara dufu
Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, ameagiza atafutwe kiungo mkabaji mwingine mwenye uwezo kama Khalid Aucho ambaye mara nyingine anapokosekana kikosini Yanga huyumba katika eneo la kiungo
"Tumeona ni kweli, misimu miwili eneo hilo linatuponza, tulifungwa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na USM Alger ya Algeria kwa sababu tulimkosa Aucho aliyekuwa na kadi"
"Hatukufanya vizuri dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini hatua ya robo fainali moja kati ya sababu ni kwamba hatukuwa na wachezaji wetu nyota wenye uwezo mkubwa akiwamo Aucho kwa sababu mbalimbali, na kuna wakati hapa alikuwa majeruhi, kwa hiyo lazima tupate mtu mwingine," kilisema chanzo
Yanga imekuwa na mahusiano mazuri na AS Maniema msimu uliopita ikimsajili Max Nzengeli
Mpaka sasa Yanga imehusishwa kuwawania nyota wawili wa timu hiyo Sangana na kiungo mshambuliaji Agee Basiala Amongo
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment