Hatutadharau mpinzani yeyote CAF CC - Ahmed
Siku moja baada ya droo ya michuano kombe la Shirikisho Afrika kupangwa, uongozi wa klabu ya Simba umesema umepokea kwa furaha ratiba ya michuano hiyo kwa kuwa wanaenda kukutana ma timu ambazo zipo chini yao kiuwezo kwenye hatua ya kwanza
Katika droo iliyochezeshwa makao makuu ya CAF, Cairo, Misri, Simba ambayo itaanzia hatua ya kwanza, inasubiri kucheza na mshindi kati ya Uhamiaji FC ya Zanzibar na muwakilishi kutoka Libya ambaye bado hajajulikana kwenye mchezo wao wa hatua ya awali
Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa njia kwao ni nyeupe kusonga mbele kwenye michuano hiyo
"Tumepokea vizuri droo ya CAF, hatuwadharau wapinzani, yoyote atakayekuja tunadili naye, kwetu tunaona njia nyeupe kwenda hatua nyingine, tunasubiri mpinzani wetu aje na tutampokea," alisema Ahmed
Alisema kwa timu yoyote itakayofuzu kwenda kucheza nao, hawatamdharau kwa kuwa ni timu ndogo kwao kwa sababu mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa
"Hizi timu ndogo hatupaswi kuzidharau, ukizidharau wanaweza kukuvua nguo ukweni, kwa hiyo tunajiandaa vizuri, kama mnavyojua tayari timu imeanza maandalizi ya Ligi Kuu pamoja na michuano hii," aliongeza Ahmed
Alisema kwa sasa kazi inaendelea kukiandaa kikosi chao kuelekea kwenye msimu mpya wa mashindano
"Mazoezi yanaanza kupamba moto kwenye kambi yetu, kila mchezaji ana morali ya hali ya juu, na kocha wetu mpya Fadlu Davids amefurahishwa na hali aliyoikuta kwa wachezaji wake"
"Kusema kweli kocha ameshaanza mazoezi na ameonesha kufurahishwa na viwango vya wachezaji aliowakuta na kusema ana kazi ya kukiunganisha ili kucheza katika mfumo anaouhitaji"
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment