Breaking: Yanga yamtambulisha Chama - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking: Yanga yamtambulisha Chama

Breaking: Yanga yamtambulisha Chama

Michuano ya EURO 2024 inaendelea pia mechi za kirafiki zinaendelea usikose kuzitazama mechi zote live bure kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote live bure pia ndani ya app yetu utaweza kutazama chanel za azam tv buree na muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Clat

Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili Kiungo Mshambulia, Clatous Chota Chama raia wa Zambia akitokea Klabu ya Simba.

Chama anajiunga na Yanga akiwa Mchezaji Huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Simba ambayo ameitumikia katika vipindi viwili tofauti.

Klabu yetu ya Young Africans imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chama raia wa Zambia.

Chama ambaye kiwango chake kimekuwa kivutio machoni mwa watazamaji amejiunga na timu yetu akitokea kwa watani zetu wa jadi hapa nchini.

Kiungo huyo ambaye ana uzoefu na soka la Tanzania, alianza kuonyesha uwezo wake hapa nchini mwaka 2018 alipotua kwa mara ya kwanza.

Ujio wa Chama katika kikosi chetu unaongeza wigo mpana katika eneo la kiungo cha ushambuliaji akiwa sambamba na Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki.


Taarifa ya Yanga; "Haya ni maboresho ya kikosi chetu katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu ujao wa 2024-2025 tukiwa na malengo ya kutetea mataji yetu yote tuliyobeba msimu wa 2023-2024 ambayo ni Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation huku pia tukihitaji kufanya vizuri zaidi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishia robo fainali msimu uliopita.

Huu unakuwa usajili wa kwanza kukamilika huku pia maboresho zaidi yakiendelea. Kaa tayari Mwananchi kwa ajili ya kufurahi zaidi."Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz