Aziz Ki amkaribisha Dube Yanga
Kama alivyofanya kwa Clatous Chama, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amemkaribisha Prince Dube 'Mwana Mfalme' ambaye Yanga ilithibitisha kukamilisha usajili wake usiku wa kuamkia Jumapili
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Aziz Ki aliweka chapisho la kumkaribisha Dube huku akimtaja kama mfungaji bora wa Ligi Kuu 2024/25
Ni wazi Aziz Ki alikuwa akisubiri kwa hamu utambulisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam Fc, akionekana kumkubali
Aziz Ki alikuwa mchezaji wa kwanza kufichua usajili wa Dube katika moja ya mahojiano yake katika mitandao ya kijamii
Aziz Ki aliweka bayana kuwa msimu ujao hana mpango na tuzo ya mfungaji bora kwani atahakikisha tuzo hiyo inabebwa na washambuliaji wa Yanga zaidi akimtaja Dube
NMsimu ujao Dube na washambuliaji wenzake katika kikosi cha Yanga washindwe wenyewe tu katika kuzifumania nyavu kwani kikosi kimesheheni wapishi wa kuwatengenezea nafasi
Chama, Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli wote watakuwa kazi moja tu, kuwatengeneza nafasi lakini pia hawataacha kufunga kama walivyofanya msimu uliopita
Post a Comment