Dirisha la usajili(FIFA Connect) kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi ya Championship, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2024/25 litafunguliwa Juni 15 na kufungwa Agosti 15, 2024.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema klabu zinatakiwa kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji katika kipindi hicho.
"Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, tafadhali zingatia muda huo wa usajili na uhamisho," imesema taarifa hiyo.
Aidha usajili na uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utafunguliwa Desemba 16, 2024 na kufungwa Januari 15, 2025.
BONYEZA HAPA KUANGALIA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA KITANDANI
Post a Comment