Kudadeki!! Mashabiki Simba waiganda 'Thank you' ya Jobe - EDUSPORTSTZ

Latest

Kudadeki!! Mashabiki Simba waiganda 'Thank you' ya Jobe

Kudadeki!! Mashabiki Simba waiganda 'Thank you' ya Jobe

Michuano ya EURO 2024 inaendelea leo mechi za kibabe zitapigwa leo usikose kuzitazama mechi hizi zote live buree kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote live bure pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za Azam tv na Dstv kudownload app hii bonyeza ðŸ‘‰ðŸ»ðŸ‘‰ðŸ»HAPA

Mashabiki Simba waiganda 'Thank you' ya Jobe

Akufukuzae hakuambii toka. Ndiyo msemo unaoweza kuutumia kwa mshambuliaji wa Simba, Pa Omar Jobe, ambaye mashabiki wa klabu hiyo wameonyesha kiu kubwa ya kutamani kuona anaachwa.

Simba wiki hii, imeanza kuwaaga wachezaji wake ambao hawatawahitaji msimu ujao, ikiwa tayari imeshawaaga wawili, aliyekuwa nahodha wake mshambuliaji John Bocco, Jumatatu Juni 17 na leo ikimuaga kiungo mshambuliaji mkongwe Said Ntibazonkiza 'Saido', wakipewa 'Thank you', yaani ahsante kwa kuitumikia klabu hiyo lakini ndani yake akatajwa Jobe.

Kila habari za wachezaji hao walipotajwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram ya klabu hiyo, mashabiki wengi wameonyesha kiu ya kusubiri 'thank you' ya mshambuliaji huyo raia wa Gambia.

Tangu atue ndani ya klabu hiyo, akiingia kupitia dirisha dogo la usajili, Jobe amefunga bao moja pekee hatua ambayo haikuwafurahisha mashabiki wa Simba licha ya kupewa muda wa kutosha kucheza ndani ya timu hiyo.


Hata hivyo, Simba italazimika kukaa mezani na Jobe kukubaliana vizuri kama inataka kukata kiu ya mashabiki wake wanaotamani aondoke, kwani mshambuliaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia klabu hiyo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz