Hizi hapa Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Hizi hapa Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga

 Hizi hapa Tetesi za usajili ndani ya klabu ya Yanga

Ligi mbali mbali zitaanza muda si mrefu download app yetu kutazama mechi zote za ligi kuu tanzania bara na ulaya live bure kabisa pia ndani ya app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za azam tv buree kabisa kudownload app yetu bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA


Jana TFF ilitangaza kuondoa kifungo cha usajili wa ndani kwa klabu ya Yanga baada ya FiFA kuiondolea kifungo kilichotokana na madai ya mshambuliaji Lazarus Kambole. Wananchi sasa wameruhusiwa kuingiza taarifa za usajili wa wachezaji wapya kwenye mfumo 

Uongozi wa Yanga umeahidi kuanzia Jumatatu taarifa zitatangazwa sambamba na mipango ya pre-season

Aidha nyota wa Yanga watatakiwa kuanza kuripoti Avic Town Jumatatu tayari kwa pre-season inayotarajiwa kufanyika nje ya nchi

Tetesi zimekuwa nyingi juu ya wachezaji ambao tayari wamemalizana na Yanga lakini uhakika ni kuwa kuanzia Jumatatu kila kitu kitakuwa hadharani

Miongoni mwa majina yanayotajwa ni pamoja na mshambuliaji George Mpole aliyemaliza mkataba na klabu ya FC Lupopo ya DR Congo

Mpole ni mchezaji wa ndani, usajili wake utakuwa maalum kuchukua nafasi ya Crispine Ngushi ambaye mkataba wake umemalizika

Aidha Yanga pia inaweza kumshusha nchini mshambuliaji Jonathan Sowah, raia wa Ghana ambaye alikuwa akiitumikia Al Nasri ya Libya

Sowah aliitumikia Medeama Fc kabla ya kutimkia Libya katika usajili wa dirisha dogo

Sowah anaweza kuchukua nafasi ya Joseph Guede ambaye mkataba wake wa miezi sita umemalizika

Guede alikuwa kwenye mipango ya kocha Miguel Gamondi lakini ni wazi mahitaji yake makubwa katika mkataba mpya yanaweza kuwa sababu ya uongozi kuamua kuachana nae

Kama kila kitu kitaenda sawa, ina maana safu ya ushambuliaji ya Yanga itakuwa na watu wa kazi kwelikweli

Kennedy Musonda, Clement Mzize bado wapo, wakiongezeka Prince Dube, George Mpole na Jonathan Sowah

Stephane Aziz Ki yupo, Pacome Zouzoua yupo, Maxi Nzengeli yupo na pengine ataongezeka yule wa bango.......!

Wananchi wanasema kwa 'mtiti' huu, kuna timu zitagoma kuingia uwanjani! Pia utakuwa aina ya usajili ambao unaakisi malengo ya Yanga ya kufanya vizuri zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujaoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz