Furaha ya Simba msimu huu iko hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Furaha ya Simba msimu huu iko hapa

Furaha ya Simba msimu huu iko hapa

Ni kesho YANGA vs AZAM FC fainali ya kisasi fainali ya kibabe unaanzaje kukosa kuucheki mtanange huu live buree bonyeza hapa kudownload app itakayo rusha mechi hii live bureeee kabisa kwenye simu yako bofya sasa kudownload mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi

Klabu ya Simba Queens inahitaji pointi tatu kupata uhakika wa kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara kwa msimu wa 2023/24.

Simba Queens inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 43 baada ya michezo 15.

Akizungumza nasi, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi, amesema malengo ni kuona timu yake inatwaa taji hilo bila ya kupoteza mechi.

“Hatuangalii mechi tunahitaji kushinda kila mechi bila ya kujali tunakutana na timu ipi. Ligi haijaisha, tusipokuwa makini tunaweza kupoteza malengo,”amesema kocha huyo.

Mgosi amesema watahakikisha wanafanya vizuri katika michezo mitatu iliyosalia ili kurejesha heshima ya klabu na kuwapa furaha mashabiki wa Simba baada ya timu ya wanaume kutofanya vizuri.


Simba Queens imebakiza mechi dhidi ya Alliance Girls Juni 07 huku wakivaana na Fountain Gate Princess Juni 10 na kisha kumaliza kazi na Geita Gold Queens Juni 14 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz