Fei Toto atoweka uwanjani baada ya Azam kupigwa na Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Fei Toto atoweka uwanjani baada ya Azam kupigwa na Yanga

Fei Toto

Leo ni ENGLAND vs BOSNIA pia GERMANY vs UKRAINE usikose kuzitazama mechi hizi live buree kwenye simu yako pia kutakuwa na mechi kati ya TANZANIA vs ZAMBIA bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hizi live kabisa bureee pia ukiwa na app hii utaweza kutazama chanel zote za azam tv na Dstv bofya sasa kuidownload pia yale mambo yetu yale yapo

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' amekimbia uwanjani na kutohudhuria zoezi la uvaaji wa medali za mshindi wa pili Kombe la Shirikisho baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya Yanga.

Feisal alionesha ishara ya kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga baada ya kufunga penati yake lakini mpaka mwisho wa mikwaju hiyo, Yanga ndiyo waliibuka mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya nne.

Klabu ya Yanga SC imetwaa ubingwa wa Kombe la FA la CRDB baada ya kupata ushindi dhidi ya Azam, mchezo uliopigwa usiku wa jana katika Dimba la Amaan Visiwani Zanzibar.



Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkali, na kushuhudia mechi hiyo kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 bila mshindi.

Mchezo huo umeamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Azam wamepata 5 na kukosa penati 4, huku Yanga wakipata penati 5 na kukosa 3.


Yanga imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba Kombe la Shirikisho la CRDB, timu ya kwanza kubeba kombe la shirikisho mara nyingi zaidi (mara 4) tangu lirejeshwe na timu ya kwanza kubeba kombe la shirikisho mara nyingi zaidi (mara 8) tangu lianzishwe.

TAKWIMU ZA FEISAL SALUM MSIMU HUU NA ULIOPITA

Feisal akiwa Yanga msimu uliopita 22|23

◉ Ubingwa ngao ya jamii - ✅

◉ Ubingwa ligi kuu - ✅

◉ Ubingwa (FA) - ✅

◉ Fainali CAF confederations cup - ✅

Feisal akiwa Azam msimu huu 23 | 24

◉ Ubingwa ngao ya jamii - ❌

◉ Ubingwa ligi kuu - ❌

◉ Ubingwa (FA) - ❌

◉ CAF Confederations cup 1st round - ❌

◉ Mapinduzi cup - ❌

◉ Muungano cup - ❌

◉ Ubingwa (FA) - ❌



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz