Dube kutambulishwa Yanga ni suala la muda tu - EDUSPORTSTZ

Latest

Dube kutambulishwa Yanga ni suala la muda tu

Dube kutambulishwa Yanga ni suala la muda tu

Mechi za EURO 2024 zinaendelea leo pia mechi za kirafiki nyingi zinapigwa leo usikose kuzitazama mechi zote live bure kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote bure pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za Azam TV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA kama utashindwa kudownload app jiunge na group letu la telegram upewe app kujiunga bonyeza HAPA

Prince Dube

Ni suala la muda tu, Prince Dube 'Mwana wa Mfalme' atatambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga baada ya kuachana na Azam Fc.

Jana Azam Fc walimkabidhi Dube 'release letter' baada ya kutimiza masharti aliyowekewa ambayo ni kurudisha fedha aliyokuwa amelipwa na Azam Fc kwa ajili ya kuongeza mkataba.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ndio iliyomaliza utata wa sakata la mkataba wa Dube ambapo awali Azam Fc walikuwa wakidai ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2026.

Kamati ilibaini mkataba ambao Azam Fc wanadai Dube alisaini ambao ungemfanya adumu katika klabu hiyo mpaka 2026, haukuwa umesajiliwa katika mfumo wa usajili FIFA Connect na hivyo Dube kutakiwa arudishe fedha alizopewa na Azam Fc ili awe huru.

Hicho ndicho kiilichotokea na sasa Dube ni mchezaji huru na anakwenda kujiunga na timu ya ndoto zake, Yanga

Safari ya Dube kun'goka Azam Fc ilianza mwezi March 2024 pale alipotangaza kuachana na timu hiyo kwa kile alichoeleza hafurahishwi vile timu hiyo inaendeshwa.

Kuondoka kwa Dube katikati ya msimu hakutofautiani na tukio ambalo aliyekuwa kiungo wa Yanga Feisal Salum alifanya Disemba 2023.


Unaweza kusema Wananchi wamejibu mapigo kwa kutumia njia ileile ambayo Azam Fc waliitumia kumn'goa Fei Toto Yanga.

Wakati Fei Toto ametoroka Yanga, uongozi wa mabingwa hao wa nchi uliweka msimamo kwa kutaka taratibu zifuatwe ikiwa ni pamoja na kuitaka timu iliyokuwa ikimuhitaji Feisal ijitokeze lakini Azam Fc hawakufanya hivyo.

Busara ikatumika kumruhusu Fei Toto kujiunga na Azam Fc baada ya ushauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan ambaye aliwataka viongozi wa Yanga kumaliza sakata la mchezaji huyo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz