Breaking: Inonga apewa 'Thank You' na Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking: Inonga apewa 'Thank You' na Simba

Breaking: Inonga apewa 'Thank You' na Simba

Mechi za EURO 2024 na COPA AMERICA zinaendelea leo usikose kuzitazama mechi zote LIVE bure kwenye simu yako download app yetu uweze kuzitazama pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za azam tv na dstv bure download app yetu sasa bonyeza ðŸ‘‰ðŸ»ðŸ‘‰ðŸ»HAPA

Henock Inonga.

Klabu Simba imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati, Henock Inonga kwenda FA Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco.

Inonga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amebakisha Mkataba wa mwaka mmoja unaomalizika 2025 lakini kutokana na klabu kujali na maslahi ya wachezaji, imemruhusu beki huyo kuondoka kwenda kujiunga na FA Rabat.

Simba imevuna dola 200,000 ikiwa ni sawa milioni 525 kwa kumuuza mlinzi Henock Inonga kwenda FAR Rabat

Inonga alijiunga na kikosi Cha Simba mwaka 2021 akitokea DC Motema Pembe ya Congo.

Katika kipindi cha miaka mitatu alichodumu ndani ya kikosi Cha Simba Inonga amekuwa muhimili wa timu na makocha wote waliopita wamekuwa wakimpa nafasi kwenye kikosi chakwanza.


Mwaka 2022 Inonga alichaguliwa mlinzi bora wa Ligi kuu ya Tanzania baada ya kuonesha kiwango bora katika msimu huo.SIMBA Yamuuza Henock Inonga

Uongozi wa Simba umemshukuru Inonga kwa utumishi wake ullotukuka katika kipindi chote alichokuwa Simba na pia imemtakia kheri katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz