Aziz Ki haendi kokote, kwa sasa anatingisha tu watu - EDUSPORTSTZ

Latest

Aziz Ki haendi kokote, kwa sasa anatingisha tu watu

Aziz Ki anabaki nyie, kwa sasa anatingisha tu watu

Leo kivumbi cha mataifa ya africa kufuzu kombe la dunia kinaendelea ambapo kenya, uganda, burundi zitashuka uwanjani na nyingine nyingi usikose kuzitazama mechi hizi zote live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayorusha mechi hizi live bure kabisa pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na dstv bofya sasa kuidownload uweze kufurahia chanel mbali mbali

Bongo pameshamnogea staa wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambaye mkataba wake na klabu hiyo umefikia tamati na sasa yuko huru kujiunga na timu nyingine yoyote au kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Kwa dalili zinazoonekana, kuna uwezekano mdogo kwa Aziz Ki kuachana na Yanga na hivyo anaenda kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao na hata mwingine zaidi.

Sababu ya kwanza ambayo inaonekana ina nguvu kubwa katika kumshawishi Aziz Ki abakie Yanga ni mzigo ambao bila shaka timu hiyo itamwekea mezani katika mkataba mpya kwa maana ya dau la kusaini mkataba pamoja na mishahara na stahiki nyingine kama vile posho na bonasi.

Yanga haipo kinyonge na kwa sasa mzigo inao hivyo haiwezi kukubali kumkosa mchezaji muhimu na tegemeo kisa kiasi cha fedha ambacho inaweza kukifikia au kukikaribia kupitia kwa vyanzo vyake hasa mfadhili na wadhamini ilionao.

Inawezekana Aziz Ki akaahidiwa dau kubwa huko nje, pia likaambatana na kodi kubwa pamoja na gharama kubwa za maisha zaidi ya zile za hapa, hivyo akaamua kuchukua mzigo wa Yanga ambao hatoutumia sana.

Ni mchezaji ambaye hana presha kubwa ndani ya timu hiyo kwa sasa na ni staa mkubwa kulinganisha na huko kwingine anakoweza kwenda ambako atalazimika kuanza upya.


Lakini hapa Tanzania jamaa ana uhuru mkubwa wa kufanya starehe bila bughudha yoyote na inasemekana tayari ameshakamata hisia za mtoto mmoja mkali wa Kibongo ambaye hali halali kwa ajili yake.

Anachokifanya kwa sasa ni kupandisha tu thamani yake ili Yanga itoe kibunda cha uhakika maana akiwahakikishia moja kwa moja kuwa anabaki, wanaweza kumchukulia poa na kutompatia kile anachokihitaji.

Jamaa amesoma Cuba kimtindo ingawa sisi tuliomtangulia darasa, tushagundua anawazuga tu ili apate maokoto ya uhakika.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz