Yanga kushusha mbadala wa Khalid Aucho - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kushusha mbadala wa Khalid Aucho

Yanga kushusha mbadala wa Khalid Aucho

Ni leo Simba vs Geita gold usikose kuitazama mechi hii live buree kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee kabisa bofya sasa

Klabu ya Yanga ipo kwenye harakati za kukamilisha usajili wa Kiungo Mkabaji wa Klabu ya AS Maniema Union raia wa Congo DR, Charve Onoya Sangana (20).

Chanzo makini kutoka nchini Congo DR kimethibitisha kuwa dili hilo linakaribia kukamilika na huenda ndani ya wiki mbili zijazo kama mambo yatakwenda vizuri basi akawa ni Mwananchi.

Chanzo hicho kimetufahamisha kuwa; "Mazungumzo yapo katika hatua za mwisho tangu Alhamisi mawasiliano mazuri zaidi yanaendelea kufanyika na naamini muda sio mrefu watamalizana"

Mazungumzo malipo ya ada usajili kwa kiungo huyo wa Ukabaji yameshaanza kujadiliwa baina ya vilabu vyote viwili yaani AS Maniema Union na Young Africans.

Yanga SC Ilipanga kusajili kiungo mwingine wa kusaidiana na Khalid Aucho na Jonas Mkude. Aucho ataendelea kusalia klabuni hapo lakini kwa lengo kuu ni usaidizi ili Khalid nae apate muda wa kukusanya nguvu mpya hasa ikizingatiwa kuwa msimu ujao Yanga watakuwa na mashindano mengi yakiwemo mawili ya Kimataifa (CFACL na AFL).

Imeelezwa kuwa, yanga wameweka mezani kiasi cha $75k ambazo ni sawa na Tshs milioni 194 kama ada ya uhamisho pamoja na nyongeza lakini mazungumzo yatajadiliwa.

Moja ya viongozi wa juu wa Klabu ya Yanga na skauti wa klabu hiyo, siku chache zijazo wataambatana na kwenda Congo DR kushuhudia Mchezo wa ligi kuu ambapo As Maniema watakuwa wenyeji.

Endapo Young Africans wakampata na Onoya basi watakuwa na Viungo 4 wa ukabaji hii ni baada ya Mudathir kubadilishiwa majukumu klabuni hapo;


Khalid Aucho

Yusuph Kagoma

Charve Onoya

Jonas Mkude.

Injinia Hersi amedhamiria kuimarisha kikosi chake na kukipanua zaidi kwa ajili ya mapambano msimu ujao.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz