Shangwe la Yanga Machinga, Kariakoo sio mchezo - EDUSPORTSTZ

Latest

Shangwe la Yanga Machinga, Kariakoo sio mchezo

Shangwe la Yanga Machinga, Kariakoo sio mchezo

Ni kesho kutwa mechi za lala salama Yanga vs Tz prison na Simba vs Jkt tanzania unaanzaje kukosa kuzitazama mechi hizi live kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayo onesha mechi hizi zote live bureeee kabisa pia kwenye app hii kuna yale mambo yetu yale bofya sasa kuidownload mapema ili kuepuka usumbufu

Baadhi ya wafanya biashara wa Machinga Complex na Kariakoo, wamesimamisha shughuli zao kwa muda wakishuhudia msafara wa Yanga ukipita, huku wanaoishabikia timu hiyo wakiamsha shangwe kubwaa.

Wafanya biashara hao,wamesimama kando ya barabara, wakiangalia mashabiki na basi lililobeba wachezaji wa klabu huyo, wakipita kwa shangwe ya kusherehekea ubingwa wao wa msimu huu.

Yanga imefanya msafara huo, kutoka Uwanjani wa Benjamin Mkapa, kupitia Keko, Karume, Kariakoo ambapo kwa sasa wanaelekea Jangwani.

Mbali na wafanya biashara hao, barabara ya mwendo kasi, yanapita magari yaliopo kwenye msafara huo, Huku foleni ikiwa kubwa.

Magari ya mwendo kasi, yamelazimika kusubili kwa muda ili kuyapisha magari hayo, kwani hakukiwa na namna ya kupenya katikati ya foleni kubwa.


Kwa sasa gari lililobeba wachezaji wa Yanga,lipo Msimbazi na askari wapo imara kulinda usalama wa raia.

Lakini mashabiki wa Simba walipo Msimbazi hawajakubali unyonge, kwani wanaimba nyimbo za klabu hiyo wakipeperusha bendera juu.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz