NBC yaiandalia Yanga sherehe za ubingwa

NBC yaiandalia Yanga sherehe za ubingwa

Ni jumamosi ya Kibabe ni jumamosi ya kihistoria huku ni Yanga vs Tabora united kesho pia ni Kmc vs Simba mechi za kibabe zote unaanzaje kukosa kutazama mechi hizi live bureeee kabisa kupitia simu yako bado unajiuliza utazitazama vipi bofya hapa kudownload app itakayorusha mechi zote hizi live bureee kabisa unasubiri nini bofya sasa kuangalia mechi zote hizi bureeeeeee

Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa sherehe maalum kwa ajili ya kukabidhi kikombe cha ubingwa wa ligi hiyo kwa mshindi, Yanga itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga itakabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kumalizika kwa mechi yao ya raundi ya 29 dhidi ya Tabora United.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa NBC, Godwin Semunyu, alisema wao kama wadhamini wakuu wa ligi tatu tofauti hapa nchini wamejipanga kuhakikisha mabingwa wote wanakabidhiwa vikombe vyao kwa hadhi na heshima wanayostahili ikiwa ni ishara ya kutambua jitihada zao.

Semunyu alisema wanaipongeza Yanga kwa mafanikio licha ya ushindani mkubwa ulioshuhudiwa kwenye ligi hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa umechochewa na maboresho ya timu shiriki kufuatia udhamini wa benki hiyo.

“Ushindani huo unachochewa kwa kiasi kikubwa na udhamini wetu kama benki kwenye ligi hizi hatua ambayo imechangia kuviwezesha vilabu shiriki kufanya maandalizi mazuri bila changamoto za kifedha. Kwa kuzingatia mazingira hayo tumeona ipo haja pia ya kushiriki kikamilifu katika kuwapongeza washindi wote wanaopatikana kwenye ligi hizi…tunawapongeza sana,’’ alisema Semunyu.

Naye Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, alisema kupitia ushirikiano na benki hiyo wameandaa tukio kubwa la kusherehekea ubingwa litakolihusisha matukio mbalimbali ikiwamo mkesha wa sherehe na ‘parade’ itakayoanzia uwanjani hadi makao makuu ya klabu hiyo.


Kamwe alisema watalitembeza kombe lao la ubingwa kwa kutumia helikopta ‘Chopper’ maalum itakayozunguka maeneo mbalimbali ya jijini ili kunogesha shughuli hiyo.

“NBC wametuheshimisha sana katika sherehe hizi wakiwa kama wadhamini wakuu wa ligi hii. Mbali na kutusaidia kufanya maandalizi ya sherehe hizi za ubingwa pia wamejipanga kuhakikisha wanasajili wanachama wetu pale uwanjani na kuwapatia kadi za uanachama za kisasa hatua ambayo ni muhimu sana hususani katika kutuongezea mapato ya klabu. Tuwashukuru sana na tunawaomba wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi siku ya tukio hilo muhimu," Kamwe alisema.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post