Klabu ya Simba inaripotiwa kutuma ofa ya Shilingi Milioni 200 Coastal Union ili kuipata saini ya beki wa kati wa klabu hiyo ya jijini Tanga, Lameck Lawi katika dirisha lijalo la uhamisho.
Awali ilidaiwa kuwa Simba SC iliwasilisha ofa ya Shilingi Milioni 170, lakini klabu ya Coastal Union iliikataa, kwa kudai ofa hiyo ilikuwa ndogo na haiendani na thamani ya mchezaji huyo.
Klabu nyingine zinazotajwa kumuwania Lawi ni Azam FC na Ihefu FC zote zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Azam FC na Ihefu FC zinazjiandaa kutuma ofa zingine tena, ili kuizidi ile ya Simba SC na kuushawishi uongozi wa Coastal Union.
Ila taarifa za kuaminika ni kuwa Lameck Lawi hajasaini karatasi zozote mpaka sasa za kimkataba katika klabu yoyote.
No comments:
Post a Comment