Mchongo mzima wa Stars kuikabili Zambia upo hivi - EDUSPORTSTZ

Latest

Mchongo mzima wa Stars kuikabili Zambia upo hivi

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco

Leo ndo leo kivumbi na jasho ni Simba vs Jkt tanzania pia Yanga vs Polisi tanzania usikose kuzitazama mechi hizi zote live bureee kabisa kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayo onesha mechi hizi zote live kabisa buree download sasa kufurahi

Kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kitakachocheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia kimeitwa kambini, lakini wachezaji wa Yanga watachelewa kujiunga nacho.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema wachezaji wa kikosi hicho watajiunga na wenzao watakapomaliza mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) utakaochezwa Juni 2, mwaka huu.

Juni 11, mwaka huu, Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo huo ikiwa kundi E kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kufanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico ambapo timu tisa kutoka Afrika ndizo zitafuzu kutoka tano za awali. Katika kufuzu yamepangwa makundi tisa na kinara wa kila kundi ndiye atafuzu.

Tayari Taifa Stars imecheza mechi mbili za kundi hilo ikianza kushinda 0-1 ugenini dhidi ya Niger mechi ikicheza Novemba 18, 2023 kwenye Uwanja wa Marrakech nchini Morocco mfungaji akiwa Charles M'Mombwa.

Mechi ya pili iliyochezwa nyumbani Stars ilifungwa mabao 2-0 na Morocco kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 21, 2023.

TIMU za kundi hilo ni Morocco, Zambia, Niger, Tanzania na Congo wakati Eritrea ikitolewa kwenye mashindano huku sababu zikiwa hazijawekwa wazi.


KIKOSI CHA STARS: KOCHA: Hemed Suleiman MAKIPA: Ally Salim (Simba), Aboutwaleeb Mshery (Yanga), Kwesi Kawawa (Syrianska FC, Sweden) na Yona Geofrey (Tanzania Prisons).

MABEKI: Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Ibrahim Bacca (Yanga), Nickson Kibabage (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Lameck Lawi (Coastal Union), Israel Mwenda (Simba), Mukrim Issa (Ihefu), Lusajo Mwaikenda (Azam), Pascal Msindo (Azam) na Nathaniel Chilambo (Azam).

VIUNGO: Novatus Dismas (Skahtar Donestsk, Ukraine), Yussuf Kagoma (Singida Fountain Gate), Morice Michael (RFK Novi Sad, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish, Misri), Feisal Salum (Azam), Mudathir Yahya (Yanga), Yahya Zayd (Azam) na Abel Josiah (TDS - TFF Academy)

WASHAMBULIAJI: Edwin Balua (Simba), Saimon Msuva (Alnajmah, Saudi Arabia), Kibu Denis (Simba), Cyprian Kachwele Whitecaps 2, Marekani), Ben Starkie (Ilkeston Town, Uingereza), Charles M'mombwa (Macarthur, Australia), Wazir Junior (KMC), Ibrahim Hamad (Zimamoto), Kelvin John (Genk, Ubelgiji), Abdul Suleiman (Azam) na Clement Mzize (Yanga).



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz