Lomalisa huyooo! Kutua zake Azam FC - EDUSPORTSTZ

Latest

Lomalisa huyooo! Kutua zake Azam FC

Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Joyce Lomalisa.

Ni kivumbi na Jasho jumapili hii ni Yanga vs Azam Fc mechi ya kibabe mechi ya kisasi ni fainali itakayo sisimua kila upande usikose kuitazama mechi hii live bureee kabisa kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayoonesha mechi hii live bure kwenye simu yako pia yale mambo yetu yale yapo

Beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Joyce Lomalisa inaelezwa anakaribia kumalizana na klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Azam FC kimesema mazungumzo baina ya mchezaji huyo yanaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa watamtangaza mchezaji huyo kuwa mali yao. 

"Mazungumzo baina ya Lomalisa na uongozi yamefikia hatua ya nzuri na wanaelekea kuafikiana, naamini wakikubaliana atasaini kwa ajili ya kujiunga na timu yetu msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.  

Alisema Azam msimu ujao imepania kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa na ndio sababu ya kuboresha kikosi chao. 

"Malengo yetu ni kufanya vema msimu ujao, tunaamini usajili tutakaoufanya utaiboresha timu yetu na kushika nafasi za juu,” kilisema chanzo hicho. 


Lomalisa alikuwa sehemu ya mafanikio ya klabu ya Yanga msimu huu baada ya kuisaidia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz