Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amebainisha kuwa kuanzia wiki ijayo wataanza kutangaza majina ya wachezaji, viongozi, na benchi la ufundi ambao wataondoka na watakaoingia kuimarisha timu hiyo.
Ahmed amesema hayo jana baada ya Ligi Kuu kutamatika huku Simba wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambapo wameangukia kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ambayo watashiriki msimu ujao jambo ambalo amesema hayakuwa malengo yao kabisa.
“Kila kitu muda wake ukifika tutaweka hadharani, kwa sasa tunamshukuru Kocha Mgunda na Selemani Matola na benchi zima la ufundi, wamefanya kazi kubwa sana kuifanya Simba kumaliza katika nafasi hiyo. Wachezaji wote wa Simba wamepambana lakini haikuwa riziki na kumaliza nafasi hiyo ya tatu.
“Taarifa rasmi, mipango yote ya Simba tutaanza kuiweka rasmi baada ya ligi kumalizika. Tuiache wiki hii ipite lakini kuanzia wiki ijayo tutaanza rasmi kuachia taarifa rasmi nani tunamuondoa.
“Simba tumemaliza ligi vibaya, mtasikia taarifa nyingi sana huyu anaondoka huyu anakuja lakini tutulie. Maamuzi ambayo tutayafanya yatakuwa sahihi kwa maslahi ya Simba,” amesema Ahmed.
No comments:
Post a Comment