Ukweli kuhusu Mzize kutakiwa na Azam FC - EDUSPORTSTZ

Latest

Ukweli kuhusu Mzize kutakiwa na Azam FC

Ukweli kuhusu Mzize kutakiwa na Azam FC

Yaani Mpaka kieleweke ni Jumamosi ya Furaha na Machozi Yanga vs Simba unaanzaje kukosa kuitazama mechi hii live bureee kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayo rusha mechi hii live bureee kabisa bofya sasa kuidownload Mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi

Mchambuzi nguli wa soka, Jemedari Said amezungumzia ukweli kuhusu dili la Azam FC na mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize.

Jumatatu tarehe 15 April 2024 uongozi wa Azam FC @azamfcofficial ulipeleka ofa kwa klabu ya Yanga SC @yangasc wakitaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Clement Mzize, ofa ya Azam FC ni Ths 400,000,000/= (400M), baada ya kupokea ofa hiyo siku iliyofuata yani Jumanne tarehe 16 April 2024, uongozi wa Yanga ukaijibu barau ya Azam FC kwamba wao kama viongozi watakaa na kujadili ofa hiyo kisha watawajibu.

Kwenye ofa ya Azam FC hakuna sehemu yoyote ambayo imezungumzia suala la kubadilishana wachezaji (swap deal) kati ya Clement Mzize na Prince Dube ambaye yupo kwenye matatizo na Azam FC.

Azam FC wamepokea maelekezo ya kocha wao kwamba anataka washabuliaji 2 mmoja mzawa na mwingine mgeni, mzawa anamtaka Mzize. Ndipo vongozi wa Azam FC wakatoka na ofa ya 400M, HAKUNA KUBADILISHANA WACHEZAJI.

Kilichotokea baada ya Azam FC kuweka pesa mezani, Mzize kaingiziwa pesa za kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga ambapo bado wapo kwenye maongezi ya mkataba mpya.


Watu wa karibu yake wamethinitisha hili na habari zinasema huenda muda wowote Clement Mzize ataongeza mkataba na Mabingwa wa nchi. Kama ana wasimamizi imara manake ni kwamba anaweza kuzoa zaidi ya 400M kutoka Yanga, Kwani Azam wako mlangoni. Ila kwa kariba ya wachezaji wetu utakuja kusikia kituko utaziba uso.

NB: Mzize anahusishwa na kutakiwa na klabu ya Watford ya England, lakini Mzize pia aliwahi kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Marseille ya Ufaransa, akili kichwani mwake na wanaomzunguka.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz