Simba siyo mali ya mtu, tumechoka na usajili wa Instagram - Kay - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba siyo mali ya mtu, tumechoka na usajili wa Instagram - Kay

Simba siyo mali ya mtu, tumechoka na usajili wa Instagram - Kay

Ni leo Jkt tanzanja vs Yanga usikose kuitazama mechi hii live bure kabisa bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee bofya sasa

Shabiki wa Klabu ya Simba na Mwanachama wa Klanbu hiyo, Kaymziwanda amesema kama Tajiri wao hanapata hasara aondoke.

Kay amesema hayo baada ya Simba kuzorota na kushindwa kupata matokeo kwa michezo minne mfululizo ikiwemo kichapo cha bao 2-2 walichopokea juzi dhidi ya watani zao Yanga.

"Haya tuanzie hapa bwana tajiri kwanza tunashukuru kwa mchango wako mkubwa sana ndani ya miaka 4 hilo kila Mwanasimba atakupongeza. Turudi ndani ya misimu hii mitatu Simba imesajili wachezaji wengi ambao kiukweli aina ya wachezaji na malengo ya timu ni vitu viwili tofauti.

"Swali kwako bwana tajiri je, unatoa hela za usajili? Na kama unatoa hao ndo aina ya wachezaji uliowataka? Kama ndio uliwataka unawekaje malengo makubwa wakati unasajili wachezaji wa kawaida ambao kihalisia hawawezi kufikia malengo ya timu?

"Na kama sio je, wewe kama mtu unaetoa fedha za usajili unaridhikaje na aina ya watu kama hao wanao kuletea wachezaji tena sio mara moja ni zaidi ya misimu 3, nini ulikiamua ukiwa kama tajiri.

"Kila siku umekuwa ukisema Simba inakupa hasara sasa tajiri kama kitu kinakupa harasa why usiachane nacho ukakaa pembeni? Halafu ukaona kama hii Simba itakufa au itapotea.

"Mara oooh tutasajili mchezaji yoyote Africa, sikia bwana tajiri mpira ni mchezo wa wazi na ni biashara pia, leo tunvaa jezi zilizo jaa matangazo yako unasemaje unapata hasara?


"Kama mpaka leo bado upo Simba basi kwa namna moja ama nyengine Simba inakufaidisha bwana Tajiri, achana kujisifu sana insta mara umefanya hivi mara vile, acha mameno mengi Tajiri toa pesa timu isajili.

"Simba inamalengo makubwa sana na wewe unajua tumechoka huu usajili wa Instagram kila mwaka weka pesa bwana timu ilete watu wa maana Mo Dewji hii Simba sio mali ya mtu ni timu ya wanachama," amesema Kaymziwanda.

Una maoni gani?Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz