Polisi yaanza uchunguzi kifo cha kocha Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Polisi yaanza uchunguzi kifo cha kocha Simba

Polisi yaanza uchunguzi kifo cha kocha Simba

Bado unatafuta app ya kuangalia mechi ya Al ahly vs Simba live buree bonyeza hapa kudownload app itakayoonesha mechi hii live bureee kupitia simu yako ni buree bonyeza sasa kuidownload mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi

Polisi nchini Rwanda wameanza uchunguzi wa kifo cha ghafla kocha wa viungo wa klabu ya APR Adel Zrane raia wa Tunisia.

Kocha huyo amefariki Dunia akiwa nyumbani kwake jana mchana ambapo kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na klabu yake ni kuwa hakuwa na dalili zozote za kuumwa na mchana wa leo alipaswa kushiriki ratiba ya mazoezi na timu hiyo.

Kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya mwandishi wa habari za michezo @mickyjnrofficial na mmoja wa viongozi wa APR ni kuwa dereva wake alimpitia nyumbani kwake kwaajili ya kumchukua kwenda mazoezini kama kawaida.

Lakini alipofika na kujaribu kuita hakuitikiwa na simu yake haikupokelewa ndipo alipowajulisha viongozi ambao baada ya kufika waliamua kuvunja mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani ambapo walikuta kocha huyo akiwa amefariki Dunia kitandani kwake.

Kwenye salamu zake za rambirambi kiungo wa zamani wa Simba SC Thadeo Lwanga alifichua kuwa aliwasiliana kwa njia ya simu na kocha huyo usiku wa kuamkia leo na alikuwa mzima wa afya


Adel Zrane amewahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa Simba SC chini ya makocha mbalimbali akiwemo Patrick Aussem.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz