Habari kutoka nchini Afrika Kusini ni kuwa Kaizer Chiefs Amakhosi4Life tawi la "Atteridgeville" mashabiki wa Kaizer Chiefs leo wataungana na Mashabiki wa Young Africans Sports Club Pretoria kwenye dimba la Loftus Stadium kuwapa hamasa (kushangilia) wachezaji wa Yanga mwanzo mwisho.
Wananchi hawana ugeni kwako kama kwao tu. Kaizer wanasema wanakumbuka mapokezi na sapoti walioipata kutoka kwa Yanga walipokuja nchini mara ya mwisho kucheza na Yanga, hivyo wapo tayari kulipa ukarimu huo hii leo.
Itakumbukwa kuwa, Klabu ya Yanga ina urafiki na mahusiano ya karibu na Klabu ya Kaizer Chiefs na ndio maana waliaalika hata kwenye Siku ya Wananchi mwanzoni mwa msimu huu.
Kaizer pia ni wapinzani wa Mamelodi ambao ndio watacheza na Yanga leo Ijumaa, Aprili 5, 2024 kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Afrika Kusini.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment