Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundonws, Rulani Mokwena amesema kuwa hatopaki basi kwenye mchezo wao wa robo fainali ya CAFCL dhidi ya Yanga SC, badala yake ataielekeza timu yake kucheza kwa kuwashambulia wapinzani wao hao.
Mokwena amesema hayo kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa huku akisisitiza kuwa ili mchezo uwe mzuri, lazima timu zote zishambuliane.
"Sitaweza kukaa nyuma ninapocheza na Yanga SC. Ili mchezo uwe mzuri ni lazima wote tucheze na tushambuliane. Yanga ni wazuri, ukikaa nyuma wanaweza kukufunga goli nyingi.
"Yanga ni nzuri inapocheza kwa sababu inawachezaji wazuri sana, ni timu tishio Afrika kwa sasa, tunajua msimu uliopita alicheza finali ya CAFCC," amesema Rhulan Mokwena.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment