Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema, faida aliyonayo kwenye mchezo wa leo dhidi ya Jwaneng Galaxy ni kutohitaji kutazama matokeo ya mtu mwingine ili kushinda.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo wa mwisho wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika, Benchikha alisema wao wamejiandaa kushinda tu na si vinginevyo.
"Sisi tunatakiwa kushinda, hatuangalii matokeo ya timu nyingine na hii ndio faida yetu, tunatakiwa kuwa imara tushinde kwa ajili ya mashabiki wetu na Watanzania wote wanaotuunga mkono," alisema Benchikha.
No comments:
Post a Comment