Huyu hapa mwamuzi wa mechi ya Yanga vs Mamelodi Sundwon CAF - EDUSPORTSTZ

Latest

Huyu hapa mwamuzi wa mechi ya Yanga vs Mamelodi Sundwon CAF

Amin Mohamed Amin Mohamed Omar.

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs MAMELODI live bure kabisa bonyeza hapa kudownload app yetu mapema ili usipitwe na Mechi hii

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mapema tu limewataja waamuzi wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali kati ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 30, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 3:00 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na CAF, mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Mohamed Omar, akisaidiwa na Mahmoud Ahmed Kamel Abouelregal na Ahmed Hossam Taha Ibrahim ambao wote ni kutoka Misri.

Mwamuzi wa akiba, atakuwa Mahmoud Nagy Ahmed Nagy Mosa ambaye naye ni raia wa Misri kama ilivyo kwa watu wa VAR, Mahmoud Ashor na Mahmoud Elbana.

Kamishna wa mchezo ni Amir Abdi Hassan kutoka Somalia, huku mtathmini wa waamuzi akiwa raia wa Angola, Inacio Manuel Candido. Gomezgani Zakazaka kutoka Malawi atakuwa ni mratibu mkuu wa mchezo, huku ofisa usalama akiwa Emmanuel Mutunami raia wa Zimbabwe.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz