Taarifa Mpya kutoka Simba ni kuhusu mechi ya Kesho - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya kutoka Simba ni kuhusu mechi ya Kesho

Kocha Simba ataja siri ya kuwafunga ASEC kesho

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema, moja kati ya faida kubwa waliyonayo dhidi ASEC kesho ni wachezaji wa wapinzani wao hao kutokuwa na mechi za kimashindano kwa muda mrefu.

Bofya hapa kuitazama mechi ya Asec vs Simba Live kupitia simu yako download app yetu Kwa KUBOFYA hapa

Matola amesema, tangu mapumziko ya AFCON, ASEC hawajacheza mechi yoyote ya kiushindani kulinganisha na wao ambao tayari wamecheza mechi kadhaa za Ligi Kuu ya NBC.

"Hii ni faida kwetu sababu wapinzani wetu wameanza mazoezi kama wiki mbili zilizopita na hawajapata mechi za ushindani kama sisi hivyo hiyo ni faida kuelekea mchezo wa kesho," alisema Matola.

Simba wapo nchini Ivory Coast wakijiandaa kuwakabili ASEC hapo kesho majira ya saa 4 usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz