Ahmed Ally azidi kuwazodoa Yanga awatupia kijembe kingine - EDUSPORTSTZ

Latest

Ahmed Ally azidi kuwazodoa Yanga awatupia kijembe kingine

Meneja wa habari na mawasiliano Simba Sc, Ahmed Ally

USikose kuitazama mechi ya Simba vs Jwaneng Galaxy live bure kupitia simu yako download app yetu Ili uweze kutazama Mechi hii Bure Bonyeza hapa sasa kuidownload Ili usipitwe

“Tunawaahidi na kuwahakikishia Wanasimba kama kuna kitu kinahitajika hata kiwe kinapatikana chini ya bahari tutakifanya ili Simba iende robo fainali. Jumamosi ni kwenda kumalizia kazi.”- Meneja wa habari na mawasiliano Simba Sc, Ahmed Ally.

“Robo fainali wamefuzu watu washambawashamba sembuse sisi. Hatuwezi kushindwa kwenda robo fainali, yani waporipori wamefuzu alafu sisi wenye mashindano tushindwe? Jumamosi saa 1 usiku tunakutana kumaliza kazi.”

“Ili timu ishinde inawahitaji Wanasimba wote, sio Mo, sio Try Again, sio Mangungu bali sisi wote kwa umoja wetu. Tutawafanya Jwaneng Galaxy kitu kibaya kama ilivyokuwa kwa Horoya.”-

“Wanasimba tukiunganisha nguvu Jwaneng hawezi kutoka salama Dar es Salaam. Robo fainali zote nne zilizopita nyie ndio mmeipeleka Simba. Kama utakuja uwanjani sio tu kushangilia bali kuipeleka Simba yetu robo fainali. Mimi naamini Wanasimba tukiamua jambo letu hakuna wa kutuzia.”- Ahmed Ally.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz