Yanga wamtoa kwa mkopo mchezaji wao Mpya Dr congo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga wamtoa kwa mkopo mchezaji wao Mpya Dr congo

  

Mabosi wa Yanga wajanja sana, baada ya kulimaliza dili la winga hatari Mkongoman, Agee Basiala kutoka klabu ya AS Maniema ya DR Congo kwa kumsainisha mkataba wa awali, kisha kumtoa kwa mkopo katika klabu hiyo hiyo ikimsikilizia kwanza.

Unaambiwaje, wakati usajili wa dirisha dogo unapokaribia kumalizika Yanga wameshafika mbali kwa kumsainisha mkataba mapema pacha wa Maxi Nzengeli, ili kuja kukinukisha kwa msimu ujao kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.

Kama utani kikosi hicho kiliamua kutuma maombi ya kumhitaji winga huyo na baadae kutuma mkataba ambapo walifanikisha, ila walibadili gia juu kwa juu na kuamua kumuacha tena hapo kwa mkopo hadi msimu utakapomalizika.


Yanga imesajili winga mpya wa kigeni aliyewahi kuichezea Simba, Augustine Okrah huku katika nafasi hiyo akichezea Jesus Moloko, Maxi Nzengeli, Augustine Okrah na kama ataingia Basiala basi inabidi mmoja miongoni mwao aondolewe.

Wakati Yanga wakiendelea kujiuliza nani abaki nani aende, winga huyo ataendelea kukipiga katika kikosi hicho cha Maniema.

Kocha wa Maniema, Papy Kimoto alisema aliambiwa na uongozi wa timu hiyo kuwa asimchezeshe winga huyo, lakini baada ya muda amepewa taarifa mpya kuwa anaweza kuendelea naye tu.

"Mara ya kwanza uongozi uliniambia watamuuza Basiala kule Yanga, lakini Jumanne (Januari 9) wameniita na kuniambia kuna mabadiliko kidogo kwamba Basiala atabaki hapa kwetu hadi mwisho wa msimu baada ya hapo ndio atakwenda huko Yanga," amesema Kimoto na kuongeza;


"Mimi kwa ile kauli ya kwanza nilikuwa simtumii tena nilijua abaki kujiandaa kwenda Yanga, lakini sasa tuko naye anaonyesha hana raha lakini atakuwa sawa baada ya muda, alikuwa ameshajiandaa kuondoka hapa."

Kocha huyo amefafanua kwa kusema; "Niliambiwa nisimtumie baada ya kupokea mkataba wa awali lakini haikuchukua muda nikapokea taarifa kuwa niendelee nae mpaka msimu utakapomalizika (June) kwani bado ataendelea kuwepo katika kikosi changu."

Kabla ya kusimama kuitumikia Maniema katika mechi alizochezea Basiala alikuwa ameshaasisti mara tano na kufunga mabao matano katika msimu huu.

Winga huyo alikuwa akihesabika kama pacha wa Maxi wakati 'Mbappe wa Congo' alipokuwa bado anaitumikia timu hiyo ya Maniema ambayo imekuwa ikizalisha mastaa wengi wa soka wanaotamba nchini humo na kiwngineko Afrika.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz