Nyota mpya wa Yanga Augustine Okrah ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga kilichorejea mazoezini mwanzoni mwa wiki hii baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili
Okrah yuko timamu kiafya baada ya kupona majeraha aliyopata katika michuano ya kombe la Mapinduzi
Kiungo huyo mshambuliaji aliyetua Yanga akitokea klabu ya Bechem United ya Ghana, anafanya mazoezi kwa ari kubwa
Okrah anafahamu haitakuwa rahisi kwake kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kama hatajituma mazoezini
Ujio wake umemuongezea machaguo ya mawinga Kocha Miguel Gamondi ambaye ndiye alieidhinisha usajili wa nyota huyo wa zamani wa Simba
Okrah pia anaweza kutumika kama namba 10, nafasi ambayo Gamondi humtumia zaidi Aziz Ki na wakati mwingine Pacome Zouzoua
No comments:
Post a Comment