Yanga kuanza na CR Belouizdad ugenini CAF CL - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuanza na CR Belouizdad ugenini CAF CL

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Novemba 25 mwaka huu mechi za hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zitaanza ambapo mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wao wataanzia ugenini huko Algeria kwa kuumana na mabingwa wenzao wa Algeria CR Belouizdad


Mtanange huu huenda ukapigwa katika uleule uwanja ambao mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho ulipigwa msimu uliopita na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya USM Alger


Disemba 02 Yanga itarejea nyumbani kucheza mechi yake ya kwanza kwa kuumana na mabingwa watetezi CAF CL Al Ahly katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa


Disemba 09 Yanga itasafiri nchini Ghana kuumana na mabingwa wa nchi hiyo, Medeama Fc na kisha tmu hizo kurudiana jijini Dar es salaam katika mchezo utakaopigwa Disemba 19 2023


February 24 2023 Yanga itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizana na CR Belouizdad na Wananchi watakwenda kukamilisha hatua ya makundi March 02 kwa mchezo dhidi ya Al Ahly


Mkakati wa Yanga ni kuhakikisha inavuna alama zote tisa nyumbani na kwenda kusaka angalau alama mbili ugenini


Hata hivyo Yanga imekuwa na rekodi bora katika mechi zake za ugenini, hii inaweza kuwa silaha muhimu katika kusaka tiketi ya kutinga robo fainaliDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz