Taarifa mpya kutoka yanga ni kuhusu Kennedy Musonda - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa mpya kutoka yanga ni kuhusu Kennedy Musonda

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda amerejea kikosini akiwa imara baada ya kupona majeraha


Musonda alianza vyema msimu kabla ya kupata majeraha ambayo yamemfanya aingie na kutoka kikosini kwa nyakati tofauti


Yanga imethibitisha kuwa Musonda amepona kwa asilimia 100, Farid Mussa akiwa mchezaji pekee ambaye anaendelea kuimarika kutoka kwenye majeraha


Unaweza kusema mshambuliaji huyo kutoka Zambia bado ana deni kubwa kutoka Wananchi kwani baada ya kuondoka Fiston Mayele, wengi walitarajia yeye kuwa ndiye mshambuliaji kiongozi


Badala yake kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekuwa akimtumia kinda Clement Mzize zaidi Musonda akikosekana baadhi ya mechi akiwa majeruhi


Jumapili ya wiki hii Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kumenyana na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC


Musonda ana kumbukumbu nzuri mbele ya Azam Fc, msimu uliopita alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mchezo ukipigwa uwanja wa Mkwakwani


Pengine hii ni mechi ambayo Musonda anaweza kuitumia kurejesha kasi yake ya kuzifumania nyavu. Katika msimu huu Musonda amefunga bao moja tu kwenye ligi kuu ya NBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz