Taarifa Mpya kutoka Yanga ni kuhusu Jonas Mkude - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya kutoka Yanga ni kuhusu Jonas Mkude

 Mkude, Metacha warejea kikosini Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Nyota watatu wa Yanga wamerejea kikosini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuivaa Azam FC, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Oktoba 25.


Metacha Mnata, Farid Mussa na Jonas Mkude hawakuhusika kwenye mechi tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matatizo ya kifamilia na utovu wa nidhamu, lakini sasa wameitwa kambini kujiandaa na mechi zijazo.


Metacha na Mkude walidaiwa kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu, huku Farid akiwa na ruhusa maalumu na kukosa mechi ya marudiano dhidi ya Al Merreikh, Ihefu na Geita Gold.


Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi aliliambia gazeti hili jana kuwa atatumia kipindi hiki cha mapumziko kuboresha kikosi chake na kuleta usawa.


"Ni muda wa mapumziko, baadhi ya wachezaji wetu wamekwenda kujiunga na timu zao za Taifa. Tutaendelea na mazoezi na hawa waliopo na lengo ni kuboresha na kuweka usawa wa kikosi chetu," alisema Gamondi aliyeifikisha Yanga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25 ikisota bila kufika hatua hiyo.


Chanzo: MwanaspotiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz